top of page

UHUSIANO WA NGOZI-KWA-NGOZI

Uhusiano wa ngozi-kwa-ngozi ni njia ya kumtunza mtoto wako. Mtoto huvaa nepi tu na ushikwa salama dhidi ya matiti yako wazi. Akina mama wanaweza kufanya ngozi-kwa-ngozi wakati wanapoanza kunyonyesha, kuanza kunyonyesha tena au wakati mwingine wowote wewe au mtoto wako unataka.
 

KUSHIKILIA MTOTO WAKO KATIKA UHUSIANO WA NGOZI-KWA-NGOZI NI MUHIMU KWA SABABU:

 • Inafanya mtoto wako ahisi salama.

 • Inakusaidia kumjua mtoto wako na huongeza uhusiano.

 • Inakutuliza wewe na mtoto wako.

 • Inaongeza usambazaji wako wa maziwa.

 • Inasaidia watoto kupata uzito.

 • Inasaidia watoto kuweka sukari yao ya damu kawaida.

 • Inaweza kumtuliza mtoto anayelia.

 • Inasaidia kuweka mapigo ya moyo ya mtoto na kupumua kawaida.

 • Inasaidia kuweka joto la mtoto wako kuwa thabiti, na ikiwa una mapacha, kushikilia pacha mmoja kwenye kila titi ufanya kila titi liwe joto peke yake, haswa vile kila pacha anahitaji.

 • Ikiwa mtoto wako alizaliwa mapema au ni mdogo sana, kuendelea na uhusiano wa ngozi-kwa-ngozi unaweza kusaidia kuokoa maisha ya mtoto.

 • Ngozi kwa ngozi husaidia watoto kuwa thabiti.

 

Akina baba wanaweza fanya ngozi kwa ngozi pia!
 

JITAYARISHE KWA UHUSIANO WA NGOZI-KWA-NGOZI

 • Vua shati lako na sidiria. Vua nguo zote za mtoto. Unaweza kuacha napi.

 • Ikiwa chumba ni baridi, unaweza kutumia blanketi kufunikia nyinyi nyote.

 • Weka mtoto katikati ya matiti yako – kifua cha mtoto kinapaswa kua kwa kifua chako. Miguu na mikono ya mtoto imeinama, kama chura mdogo.

 • Hakikisha mtoto anaweza kupumua - shavu la mtoto kwenye ngozi yako. Kichwa cha mtoto kinapaswa kuwa karibu kutosha kumbusu.

 • Kaa kitini au kwenye kitanda chako. Hakuna mito au shiti za ziada zinapaswa kuwa karibu na mtoto.

 

NGOZI KWA NGOZI KWA KILA MZAZI NA MTOTO

Je, ni salama? Ndio, ikiwa wewe na mtoto mko katika nafasi sahihi na hakuna matandiko ya ziada au mito.

Je! Ninaweza kufanya ngozi-kwa-ngozi na mapacha? Ndio, ukiwa na mtoto mmoja kwa kila titi, bado unaweza kufanya ngozi kwa ngozi.

Nakama sijisikii vizuri? Mruhusu mtu ajue ikiwa haujisikii vizuri ya kutosha kushikilia mtoto wako.

Nakama mtoto wangu amezaliwa mapema? Unaweza kufanya ngozi kwa ngozi kusaidia kuthibiti mtoto wako.

Naenza anza lini ngozi-kwa-ngozi? Unaweza kuanza mara tu mtoto anapozaliwa.

Je! Ninaweza bado kufanya ngozi kwa ngozi ikiwa mtoto amekua? Ndio, ngozi kwa ngozi ni muhimu hata kwa watoto wakubwa.

Je! Ngozi kwa ngozi inaweza kusaidia kutengeneza maziwa zaidi? Ndio, ngozi-kwa-ngozi inaweza kusaidia mtoto wako kushikilia na kunyonya vizuri zaidi. Ikiwa mtoto ananyonya wakati wa ngozi kwa ngozi, matiti yako itatengeneza maziwa zaidi.

bottom of page