top of page

KURUDI KAZINI AU SHULENI

Unaweza kutaka kuendelea kunyonyesha wakati unafanya kazi au unarudi shuleni kwa sababu nyingi: ndio chakula bora kwa mtoto wako, inalinda mtoto dhidi ya magonjwa na ni njia ya kuungana tena unaporudi nyumbani.

Kanuni ya Mazoezi mema ya Afrika Kusini juu ya Ulinzi wa Wafanyikazi wakati wa ujauzito na Baada ya Mtoto Kuzaliwa [1] hukupatia huakikisho wa mapumziko ya kunyonyesha ya dakika 30 mara mbili kwa siku, kwa uuguzaji au ukamuaji wa maziwa kila siku ya kufanya kazi, kwa miezi sita ya kwanza ya maisha ya mtoto. Akina mama wanaofanya kazi nawananyonyesha uchukua muda kidogo kutoka kazini ili kutunza watoto wagonjwa.

MAHALI KAZINI AU SHULENI KUKAMUA

Je! Kuna eneo la kibinafsi lililo na mlango ambalo linawezwa kufungwa? Kama hakuna, unaweza kuleta skrini kwa ubinafsi ama uvae kifunikio unapokamua.

Je! Kuna jokofu la kuhifadhia maziwa yako? Kama hakuna, utahitaji kuleta barakoa yako iliyoundwa kwa io kazi iliyo na matofali ya barafu.

Akina mama wengine hutumia sehemu ya chakula chao cha mchana au mapumziko ya chai pamoja na mapumziko ya kunyonyesha yanayotolewa na Kanuni ya Mazoezi mema ya Afrika Kusini. [1]

 

KIASI CHA MAZIWA

Acha angalau 30-40 ml ya maziwa yako kwa kila saa ambayo uko mbali na mtoto. Wakati mwingine mtoto anaweza kuhitaji zaidi ikiwa mtoto anapitia ukuaji.

KUHIFADHI MAZIWA YAKO

Mama wengi ukamua maziwa kazini leo ili waache na mtoto kesho.

Vyombo vya glasi ni nzuri na vinaweza kutumika tena. Mwosho moto wa sabuni ndio yote ambayo inahitajika kua na mtoto mwenye afya kamili.

Weka maziwa yako baridi ikiwa hauitumii katika masaa machache yajayo.

Ikiwa unahifadhi maziwa ya kutumia baadaye, unaweza kuyachanganya pamoja mara moja yakiwa kwenye joto sawa.

Hifadhi maziwa katika mafungu madogo ya 60-100 ml ili kuepuka kuiaribu.

SIKU ZA KWANZA KURUDI KAZINI

Utamkosa mtoto wako na mtoto wako atakukosa. Tenga muda asubuhi kwa uuguzi kabla ya kuondoka.

Ongea na mlezi wa mtoto juu ya kuacha maziwa yako na jinsi mtoto wako atakavyolishwa (kwa mfano, chupa au kikombe cha plastiki).

Lete picha ya mtoto wako kuangalia au kipande kidogo cha nguo ili kunukia wakati wa kukamua maziwa yako.

Vaa shati linalokusawazisha au lenye vifungo mbele ili kufanya kukamua maziwa kuwe rahisi.

Mtoto wako anaweza nyonya zaidi usiku ili kulipia wakati ambao alikua mbali na wewe. Mama wengi humweka mtoto karibu usiku ili kupata mapumziko zaidi. Vile mtoto anaweza kuuguza mkiwa pamoja, ndivyo mwili wako utatengeneza maziwa zaidi.

 

KUTUMIA MAZIWA YAKO

Watoto wengine wanafurahi kunywa maziwa baridi, au unaweza kupasha chombo moto kwenye bakuli la maji moto. Husipashe moto maziwa moja kwa moja kwenye jiko au kwenye microwave.

Maziwa ya mabaki yanaweza kupeanwa wakati wa kulisha ujayo.

Ikiwa maziwa yaligandishwa, husiyagandue tena mara tu yanapotakaswa, na uitumie ndani ya masaa 24.

Maziwa yaliyowekwa kwenye baridi na maboksi ya barafu yanaweza kutumika ndani ya masaa 24.

Maziwa yaliyowekwa nyuma ya jokofu yanaweza kutumika ndani ya siku 3-8.

Maziwa yaliyowekwa kwenye sanduku la barafu la jokofu yanaweza kutumika ndani ya wiki 2.

REFERENCES

[1] The Basic Conditions of Employment Act (BCEA) of South Africa

- https://www.gov.za/documents/basic-conditions-employment-act

and

The “Code of Good Practice on the Protection of Employees during Pregnancy and after the Birth of a Child” COGP)

- http://www.labour.gov.za/DocumentCenter/Pages/Home.aspx 

bottom of page