top of page
KUNYONYESHA NA MATUMIZI MABAYA YA MADAWA YA KULEVYA
Kunyonyesha uhakikisha mtoto wako yuko na afya ya kawaida, ukuaji na maendeleo ya ubongo. Kama unatumia madawa au matibabu, ni muhimu kufahamu jinsi haya yanavyoweza kuathiri maziwa na mtoto wako.
MATIBABU
Wamama kwa mara huwa wanaambiwa hawawezi kunyonyesha wanapopata matibabu. Kwa mara nyingi hili sio kweli, na matumizi ya maziwa bandia kuna hatari. Kabla uache kunyonyesha, tafuta taarifa zaidi kwa kuwasiliana na La Leche League Afrika Kusini. Unaweza fanya utafiti kuhusu usalama wa dawa kwa www.e-lactancia.org.
NIKOTINI (TUMBAKU)
Nikotini iliyo kwa damu yako inaongeza uwezekano wa hatari ya kumwachisha mtoto kunyonya na kutokuwa na maziwa mengi. Watoto waliozaliwa na wavutaji sigara wako na uwezakano wa juu wa kuwa na msokoto wat umbo na SIDS (Ugonjwa wa Kifo kwa ghafla cha watoto wachanga).
Ikiwa huwezi kuacha uvutaji sigara, ni njia salama pia kumnyonyesha mtoto ukitumia maziwa bandia.
Punguza uvutaji sigara na uvute sigara pindi tu baada ya kunyonyesha badala ya kabla.
POMBE
Pombe huingia kwa haraka ndani ya damu ya mama na maziwa yake pia, na kuhathiri kwa pakubwa mama na mtoto. Kulewa kusio kwingi si mbaya, sanasana ikiwa mtoto amepitisha umri wa wiki nane na unyonyeshe kwa muda uliopita masaa mawili baadaye. Kulewa kwa wingi kunaweza sababisha kulia, kutonyonya sana and kukua polepole, na kunaweza athiri jinsi ubongo wa mtoto anavyokua. Matumizi ya pombe pia kunaweza athiri jinsi unavyomtunza mtoto wako. Fahamu kuwa unavyolewa sana, ndivyo pombe inavyokaa kwa mwili wako.
KOKEINI NA SAUTI
Kiasi kingi cha dawa hii upenya ndani ya maziwa ya matiti na mbaya kwa watoto. Moshi kutoka kwa sauti inayotoka kwa kokeini pia inaathiri vibaya mtoto wako. Mama wanafaa kungoja angalau masaa 24 baada ya kutumia kokeini kabla ya kunyonyesha.
BANGI (DAGGA)
Kuna tafiti chache kuhusu athari za dagga. Kuna uwwezekano wa kuwa na madhara ya muda mrefu kwa ubongo wa mtoto wako. Baada ya matumizi mengi, watoto huwa na dagga kwa miili yao kwa wiki kadhaa. Mama hawafai kutumia dagga wakati wanaponyonyesha.
Ikiwa mtu mwingine kwa familia yenu hutumia dagga, wanafaa kuitumia wakiwa mbali na mtoto.
METHAMPHETAMINE (TIK) AND CRYSTAL METH
Madawa haya hutawala na ni shida inayoongezeka kwa nchi nyingi. Hakuna habari nyingi jinsi tik inavyoathiri ukuaji na afya ya mtoto, lakini tunafahamu inahusishwa na matatizo ya jinsi anavyotangamana kijamii, unyanyasaji wa kinyumbani na kiwango duni cha kunyonyesha.
Ikiwa wewe ni mama anayenyonyesha na umetumia tik, inafaa ungoje angalau masaa 48 kabla ya kunyonyesha tena au ambapo methamphetamine haitagundulika wakati unapopima mkojo. Unaweza kamua na kutupa maziwa yako kwa sasa ili kudumisha uzalishaji wa maziwa.
bottom of page